IVECO: UZINDUZI WA TRAKKER

Gia ya kimkono kwa muda mrefu, imekuwa kawaida kwa magari mazito ya kibiashara kwenye Mashariki Kati. Hata hivyo, watengezaji sasa wanashinikiza msukumo kuelekea kwa gia boksi za kujiendesha, na sekta inaanza polepole kuona faida hizo.

Kulingana na mwenendo huu unaokua, hivi karibuni Iveko ilizindua Trakker Eurotronic kwenye tukio la uzinduzi lililofanywa Dubai Autodrome hapo mji Motor, lililofanywa kwa kushirikiana na muuzaji wake wa UAE, Saeed Mohammed Al Ghandi & Wana (SMAG). Ilihudhuriwa na wateja 150 kutoka sehemu mbalimbali za emirati, wakiwakilisha manispaa, kampuni za ujenzi, machimbo, waendeshaji usafiri na shughuli nyengine.

Baadhi ya aina tofauti za Trakker zilizochaguliwa zilikuwa kwenye maonyesho, na nyota ya maonyesho hayo, yalikuwa pamoja na modeli nne za Trakker AD380 zenye miundo tofauti: tipa, kompakta, tanka la maji, kichanganyo. Waliohudhuria walipewa fursa ya kujaribu Trakkerkwenye njia na kupitia utendaji kazi wa gari hili wao wenyewe.

Mbali na Trakker, magari mengine kutoka orodha ya Iveco yalikuwa kwenye tukio hili, yakiwemo Eurocargo na iliyo mpya Daily.

Kuanzisha gia boksi ya kujiendesha kumekuja wakati soko linazidi kufahamu usalama na gharama ya jumla ya umiliki, anaeleza Graham Turner, Mkurugenzi Mtendaji wa Al Ghandi Auto. “Tunazungumzia kuhusu trakta ya nafuu zaidi kiuchumi kufanyisha kazi,” anasema, akiashiria kuwa gia boksi ya kujiendesha si tu rahisi kwa dereva, bali pia inahusisha ukarabati na kudhoofika klachi kwa kiasi cha chini zaidi.  

UAE kwa ujumla inaenda kuelekea kwa viwango zaidi vya usalama barabarani kwa magari ya kibiashara, Turner anasema. “Tunaona mipango mingi ya serikali yanayopitia hatua za majaribio, kupitia programu za usalama na nyenginezo, ni fursa kwa kampuni zote zilizoko hapa kuwekeza kwa wakati ujao.”

Badiliko kuelekea kwa gia boksi lilianza takriban miaka 10-15 iliyopita kwenye eneo la EMEA, anasema Luca Sra, mkurugenzi wa kibiashara – Afrika na Mashariki Kati hapa Iveco.  “Umekuwa mwenendo ambao unaendeshwa kiasili na nchi za Ulaya kama UK, Ujerumani, Ufaransa, ambao ukasambaa kwa nchi za Ulaya kusini na sasa unakuja hapa.”

“Mawazo kama gharama yote ya umiliki, umadhubuti wa magari pamoja na athari ya mtindo mbaya wa kupeleka gari kwa draivulaini, mfumo wa kupiga breki na matumizi ya fueli inazidi kuwa maarufu zaidi.”

Kwa hivyo, Trakker Eurotronic mpya itafaidisha vyema mapato ya wateja wa Iveco kwenye eneo na kwenye UAE, anasema. 

Pamoja na kuanzisha gia boksi ya Eurotronic, mkusanyiko wa Trakker ni mpana kuliko hapo awali na unajumuisha injini za Cursor 13 na kabini mbili (Hi-Land na Hi-Track). Toleo za malori madhubuti zinapatikana  kwa mitindo ya 4×2, 4×4, 6×4, 6×6, 8×4 na 8×8 ikiwa na vipimo vya nguvu kwanzia 380hp hadi 440hp.

Gia boksi ya kujiendesha ya EuroTronic inaweza kutumika kwenye mtindo wa kujiendesha kamili au kujiendesha nusu. Shifti ya gia inapigiwa hesabu kulingana na hali ya mzigo, hali ya barabara na mtindo wa kuendesha gari, kuboresha utendaji kazi wa gari, matumizi ya fueli na utulivu.

Upesi wa gia unalinganishwa kwa kukubaliana kielektroniki na upesi wa injini, ambao ni haraka zaidi kuliko kulinganisha kwa msuguano. Dereva akipenda kubakisha uwiano huohuo kupitia njia ngumu, anaweza kuswichi kwa mtindo wa kujiendesha nusu kudhibiti mabadiliko ya gia.  

Gia boksi ya Eurotronic imeundwa na ZF pamoja na Iveco, alibainisha Sra. “Malori yetu yametengezwa na mikakati ya ubunifu shirika na hivyo, huwa tunatafuta washiriki bora zaidi ili kutupatia suluhisho bora zaidi. Hii ndio sababu ZF imechaguliwa. Ni kampuni ya kisasa zaidi na mtoaji.”

Trakker

Trakker ni nyota ya  Iveco kwenye nyanja nje-barabara ya kazi-nzito, na inapatikana na uzito wa gari wa jumla (GVW)unaoanzia kutoka  18-41t na uzito wa mkusanyiko wa jumla wa hadi 70t. Kwa ziada, Trakker mpya inatoa kabini yenye asili ya Stralis ambayo inachanganya kiwango cha utulivu cha kwenye-barabara na utendaji kazi wa nje-barabara. Iveco imefanya kazi sana kwenye utulivu wa dereva kwenye kabini ya Trakker mpya, haswa kwa masuala ya mfumo wa springi na kunyonya mishtuko, utulivi kitini na agonomiki ya dashibodi, Sra anasema.

Biashara kwenye eneo pana la Mashariki Kati na Afrika na pia la Emirati inakua, yeye na Turner walidokeza. 

“Eneo la Afrika na Mashariki ya Kati ni mnunuzi mkubwa wa Trakkers,” Sra anasema, akiongeza kuwa eneo hilo ndio mojawapo ya misingi mikubwa zaidi ya wateja kwa Iveco Trakkers. “Ndani ya eneo hili, tunapeleka zaidi au chini ya idadi 5,000 kila mwaka.”

Licha ya kufaa nje ya barabara, Trakker pia ni kawaida kutumika hapa na pale kwenye eneo, haswa kwenye soko za Afrika Kati, kwa usafiri. “Kwenye nchi kama Djibouti, Ethiopia, Nigeria na Angola, kawaida inatumika kama kabu muundo pamoja na mwili wa mizigo wa kubakia na trela-nusu ilioambatanishwa.” 

Kwenye UAE, kuna mahitaji yanayoongezeka kutoka kwa kazi za machimbo, haswa miradi ya majengo inaanza Emirati na Qatar. “Qatar inachukua mali ghafi yake nyingi kutoka Fujairah,” Turner anasema, akilekeza kuwa mahitaji kutoka Qatar yalianzisha miradi mengi ya sekta ya kukokota bidhaa nzito  ya UAE miaka kadhaa iliyopita. 

Miradi inayokuja kama eneo la Expo 2020 Dubai inamaanisha kuwa UAE inapangwa pia kuwa mteja mkubwa kwa miaka michache inayokuja, anaongeza. “Ni wazi kuwa soko bado linaweza kuwa tata, na athari za 2009 bado hazijaondoka kabisa. Lakini sasa tunaona ongezeko kuelekea 2020, kwa hivyo ni kama bembea kwa kiasi kidogo.

“Kwa hivyo, ni muhimu kwetu kuwa tuna mkusanyiko mkubwa wa bidhaa kwa ajili tuna kila kitu kutoka matatu ndogo kupitia njia yote hadi malori mazito na ni waaminifu kwa huduma yetu na programu zetu za ukuaji na mafunzo.”

Kwa kutarajia ongezeko la wakati ujao, SMAG ina maeneo mapya yanayoendelezwa Emirati Kaskazini, kuwa karibu zaidi na wateja wake. “Fujairah, kutakuwa na ongezeko kwenye aina tofauti ya machimbo, usongeaji mwingi wa mizigo na kadhalika, kwa hivyo tunaenda kuelekea pale ambapo wateja watakuwepo.”

Utoaji hewa chafu na fueli badili

Wakati malori yanayoletwa kwa sasa ni Euro 3, Ivaco imekuwa ikipokea maombi zaidi na zaidi ya malori ya Euro 5, anasema Marco Torta, msimamizi sehemu wa eneo la Gulf hapo Iveco. “Wasiwasi tu uliopo ni uzuri wa dizeli hapa UAE. Lakini tayari tumeanza kuleta vifaa vya Euro 5. Wakati ujao, tutakuwa na magari ya Euro 5 zaidi na zaidi, hasa kwa kutumiwa na manispaa.’

Sra anabaini kuwa mtengezaji pia amekuwa akifanya kazi na Mamlaka ya  uwekaji Viwango na Upimaji ya Emirati (ESMA) kuboresha uzuri wa fueli inayoletwa UAE. Hata hivyo, uzuri wa fueli ni suala linalozuia magari yanayoendeshwa na fueli badili kukubalika zaidi kila mahali kwenye UAE, Torta na Sra wanasema.

Licha ya masuala haya, kampuni imekuwa ikiona hamu zaidi ya fueli badili, Sra akibainisha kuwa amepokea ulizio la magari yanayoendeshwa na CNG. Karibuni tutaonyesha baadhi ya injini badili mpya hapa kwenye soko la UAE.”

Iveco imejihami vizuri kukidhi mahitaji ya injini badili, na inatoa mitambo-nguvu badili kwenye mkusanyiko wake wa magari ya kibiashara zisizo nzito na za kati. “Tuliingiza injini za CNG zaidi ya miaka 20 iliyopita, tukianza na mkusanyiko Daily. Tuko tayari na suluhisho mseto na karibuni tutakuwa na za kiumeme pia. Kwa ziada, karibuni tuliingiza gari la LNG.” Sra anasema.

“Hii ni sehemu ya mkakati maalum uliowekwa miaka iliyopita na kampuni ili kumakinikana fueli badili.”

Mafunzo na gharama yote ya umiliki

Ni ngumu kwa mtengezaji wowote wa  gari la kibiashara kupanua soko lake bila kuwa na mkakati madhubuti wa baada ya mauzo. Kwa Iveco na SMAG, sehemu muhimu ya utoajai wake wa baada ya mauzo ni programu za mafunzo za wauzaji na wateja.

SMAG ilifungua kituo chake chenyewe miaka michache iliyopita kutoa mafunzo ya aina tofauti, ya vifaa, huduma na kadhalika, Turner anasema, akibainisha kuwa Iveco inatumia vituo hivyovhivyo kufanya mafunzo kwa wauzaji, wateja na mafundi kwenye maeneo ya GCC. “Tuna chumba cha mafunzo cha mtindo-darasa, chumba kidogo zaidi na cha karibu zaidi, na sehemu ya mafunzo ya karakana pia, kwa hivyo tunaweza kufanya aina zote za mafunzo sisi wenyewe. Tuliamua kufanya kituo hicho kipatikane kwa washiriki wetu wote pia.”

“Watu wanapanda ndege kuja kutoka Saudi au Kuwait kupewa mafunzo kwenye  kituo chetu cha mafunzo. Kikweli, ni sehemu ya kujitolea kwetu kwa ushirikiano wetu lakini pia ina faida za muda mrefu pia. Mteja akitunza vizuri bidhaa zetu, atarudi kununua zaidi.”

Mafunzo kwa wateja na madereva ni sehemu ya mkakati wa kabla ya mauzo wa Iveco na yanasaidia chapa kutoa gharama jumla ya umiliki ya chini zaidi, Sra anabainisha. 

“Tulipoanza kuwafunza madereva, athari ya matumizi ya fueli kabla na baada ya mafunzo ni muhimu. Unaweza kufikisha tofauti ya matumizi ya fueli kati ya 5-15%. Wamiliki hawakuweza kuamini .”

Source : Me Construction News